Ushindani NAMIMI NIPO

Kuhusu ushindani

NAMIMI NIPO shindano la uchoraji, sanaa za mikono na ugunduzi wa kisayansi kwa njia ya mtandao ni shindano linalolenga kutafuta na kuwahamasisha vijana kutumia vipaji vyao na ujuzi walionao katika kubuni na kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vitawasaidia kukua kibiashara. Mradi huu ni muendelezo wa mradi mwingine wa Arts and sports to keep Tanzanian kids in school ulioendeshwa na FASDO mnamo mwaka 2011 katika shule sita za msingi jijini Dar es Salaam. Mradi huu ulifanikiwa kufanyika katika awamu za awali tu ambapo shule sita zilipewa computer na semina za michezo. Hatua ya mwisho ya mradi ambapo ilikuwa ni kufanya mashindano ya shule na shule ya sanaa na michezo haikufanikiwa kufanyika kwa sababu ya muingiliano wa ratiba kati ya shule na ratiba za kiserikali (Baadhi ya wanafunzi na walimu walikuwa wanashiriki HALAIKI kwa ajili ya kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania) na ushirikiano usioridhisha kutoka kwa walimu wa michezo. Kupitia shindano hilo na uzoefu tuliopata , FASDO imebuni shindano hili la uchoraji, sanaa za mikono na ugunduzi wa kisayansi kwa njia ya mtandao ambalo linafanyika Tanzania nzima na kuwahusisha vijana wenye umri wa miaka 12 – 24 wanaosoma na wasiosoma. Pamoja na hayo ongezeko la vijana wanatumia mtandao imechangia kufikia maamuzi ya kuendesha shindano kwa njia ya mtandao. Pia tafiti zinaonyesha pamoja na ukuaji wa teknolojia (matumizi ya mtandao) vijana wengi wa kitanzania hawatumii mitandao kama fursa ya kujikwamua katika hali ngumu ya maisha.hivyo basi shindano hili linalenga kuhamasisha vijana kutumia mitandao na vipaji walivyonavyo kujikwamua katika hali ngumu ya kiuchumi na kukosa ajira.

Vigezo vya Ushiriki

Shindano hili ni kwa ajili ya watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 12 - 17 na 18 - 24 tu. Tathmini ya kazi ya sanaa itaangalia mambo yafuatayo:

 • Upekee wa kazi na ujumbe : watatakiwa washiriki wawe wabunifu wawezavyo! Wawe huru kuwakilisha mawazo yao kupitia sanaa !
 • Kazi zao ziendane na tamaduni na mila za kitanzania ( iwe inayoweza kuchapishwa na inayofuata maadili ya kitanzania).
 • Isiwe imewahi kuonyeshwa sehemu nyingine au kutumika katika shindano lingine.
 • Iwe kazi yake binafsi kwa asilimia 100 (ameibuni yeye mwenyewe) –hivyo basi usaidizi wa mzazi au mlezi au mtu yeyote uwe ni katika kumsaidia kijana huyu katika kumpa vifaa tu. Ikijulikana amenakili kazi ya mtu sheria itafuata mkondo wake.
 • Kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18 mwalimu au mzazi atatakiwa ajaze fomu ya ridhaa na kuituma pamoja na kazi ya mshiriki kupitia barua pepe namimi-nipo@fasdo.org
 • Kila mshiriki atashiriki katika kipengele kimoja tu.

ANGALIZO: Vigezo vingine vya ushiriki vimewekwa katika vipengere vya ushindani. 

Muongozo

 • Namna gani ya kushiriki?
 • Katika kazi yako andika kichwa cha habari na maelezo kidogo ya kazi yako.
 • Ushiriki utafuata masharti na vigezo vya mashindano.

Tarehe za Mwisho

 • 15 March: kujisajili
 • 31 March: kutuma kazi
 • 20 April - 03 May: kura za mtandaoni
 • 04 May: kumtangaza mshindi

Zawadi

 • Katika kila kipengere kazi mbili nzuri kuliko zote itajishindia dola za kimarekani 300. Moja kwa vijana wenye umri (12-17) na nyingine kwa vijana wenye umri(18-24).
 • Washindi 20 wa kwanza watapatiwa mafunzo ya sanaa na ujasiriamali kwa siku tatu. Mafunzo haya yatafanyika Makao makuu ya FASDO, Dar es Salaam.
 • Washindi 20 wa kwanza watapata nafasi ya kukutana na watu waliofanikiwa kupitia sanaa kama wachoraji maarufu Tanzania, wanamitindo mbalimbali, watengenezaji wa kazi mbalimabali za sanaa.
 • Washiriki wote watapewa nafasi ya kutangaza kazi zao bure kwa mwaka mzima katika tovuti  ya FASDO, ukurasa wa facebook , FASDO TV, FASDO blog,  ukurasa wa instagram na Twitter wa FASDO.
 • Tuzo zote zitatolewa katika sherehe kubwa itakayofanyika makao makuu ya FASDO, Dar es salaam. 
Go to top