Sayansi na ugunduzi wa kiteknolojia

Vijana na watoto mara nyingi huwa ni wabunifu, wenye hamu ya kujua mambo kindani zaidi. Tunatafuta watoto na vijana kama hawa ili kuwalea/ kuwakuza wawe watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na watatuzi wa tanzania, Africa na dunia kwa ujumla.

Shindano hili linalenga kutengeneze mtazamo mpya kwa matokeo chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla. Tunalenga kuunda mfumo wa kufundisha matumizi ya njia za asili na njia nyingine za habari kuhamasisha vijana kutengeneza bidhaa kwa ajili ya matumizi katika kizazi hiki kipaya cha sayansi na teknolojia na kutenegeneza mtandao wa ajira.

Washiriki watatukuwa ni kijana au motto yeyote mwenye kipaji na ujuzi awe mwanafunzi au siyo mwanafunzi, mwenye ndoto ya kutengeneza vitu vya kisayansi ambapo vitahusisha masula ya hesabu, kemia, biolojia na fizikia.

Kumbuka:

 • Usifungwe na mawazo/ideas zilizopo za miradi ya sayansi.
 • KUTUMA: Tafadhali tutumie picha ya kazi yako. Picha na kazi yako halisi vitunze. Kwani vitahitajika baadaye pale kazi yako itakapochaguliwa.
 • Maelezo ya kazi yawe na:
  • Utangulizi mfupi  kuhusu kazi nzima
  • Hamasa/ elezea tatizo ulikokuwa unataka kulitatua
  • Maswali na bunio
  • Mchakato mzima wa utengenezaji (vifaa pamoja na hatua ikiwemo majaribio yaliyofanyika)
  • Matokeo: maelezo juu ya matokeo hayo
  • Mwisho
  • Mapendekezo, muonekano, maombi ya baadaye
 • Tafadhali tuma picha ya bango na/au mfano/sampuli (inapobidi)

Jisajili hapa !

Fomu ya usajili

Je umekwisha jisali? Sasa uko tayari kututumia kazi yako !

Fomu ya kutuma

Go to top