Sanaa za mikono

Vijana na watoto katika kipengere hiki watatakiwa kubuni kazi zao kwa kutumia malighafi zinazopatikana maeneo waliyopo. Washindani watatakiwa kutengeneza kazi tatu kutoka katika kipengere chochote hapo chini:

  1. Sanaa za mikono za kutumia miti kama vinyago (mfano vinyago vya kimakonde n.k)
  2. Sanaa za mikono kutumia mifupa, mawe, vioo au chuma mfano decorated sea shells.
  3. Mapambo ya nyumbani ( vikapu vya urembo, mikeka, kapeti, vya kuwekea sabuni na vingine vingi)
  4. Sanaa za mikono kutumia udongo kama vyungu vya maua n.k

Kumbuka:

  • Jitahidi kazi yako iwe ya mvuto na ya kipekee.
  • KUTUMA: Tafadhali tutumie picha ya kazi yako. Picha na kazi yako halisi vitunze. Kwani vitahitajika baadaye pale kazi yako itakapochaguliwa.

Jisajili hapa !

Fomu ya usajili

Je umekwisha jisali? Sasa uko tayari kututumia kazi yako!

Fomu ya kutuma

Go to top