Kuchora na kupaka rangi

Wachoraji wengi wenye mafanikio makubwa walianza kuchora wakiwa na umri mdogo . tofauti kati ya wachoraji wenye mafanikio na wengineo ni kwamba wao waliweza kupata na kuona fursa wakati wengine wakiwa hawana habari. Kipengere hiki kinalenga katika kusaidia vijana wenye kipaji cha hali ya juu kuweza kuona fursa ambazo ziko mbele yao na namna wanavyoweza kutumia malighafi za hapa nyumbani/zilizopo maeneo ya kwao katika kutengeneza kazi mbalimbali za kibunifu/kisanaa.

Kila mshiriki atatakiwa atume kazi isiyozidi moja katika vipengere hivi:

  • Uchoraji: picha ambayo imechorwa kwa mkono ambayo ni aidha nyeupe au nyeusi katika mlalo ulionyooka (Unaweza kutumia Penseli, wino, mkaa, pastel, picha za rangi, scratchboard, marker peni etc)
  • Upakaji Rangit: Ubunifu wa kupaka rangi katika mlalo ulionyooka kwa kutumia mafuta, akriliki, rangi za maji, gouache, tempera, ink, encaustic, fresco, spray paint, etc. ipakwe kwenye canvas, canvas board, karatasi au sehemu yoyote iliyoonyoka

Kumbuka:

  • Picha zilizochukuliwa kutoka mtandaoni au zilizochapishwa tayari hazitakiwi hazitapokelewa na mtu akituma atatolewa maramoja kutoka mashindanoni.
  • Picha ziwe na ukubwa wa A4 hadi A0.
  • KUTUMA: Tafadhali tutumie picha ya kazi yako na kuhifadhi picha halisi. Tutahitaji baadaye.

Jisajili hapa !

Fomu ya usajili

Je umekwisha jisali? Sasa uko tayari kututumia kazi yako!

Fomu ya kutuma

Go to top