Mwandishi wa Filamu Kijana

Mwandishi wa Filamu Kijana

Kati ya vipengere vya mashindano ya Bongo Style Competitiion 2017 ni kipengere cha shindano la uandishi wa filamu fupi kwa vijana chini ya umri wa miaka 28. Kipengere hiki kitawakutanisha vijana wenye vipaji na wabobezi katika uandishi wa filamu fupi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania ambao watashindana kujipatia zawadi ya Milioni Moja na fursa nyingine za kukua katika sekta ya filamu duniani.

Mshiriki katika kipengere hiki inatakiwa awe:

  • Mtanzania kwa uraia
  • Mwenye umri chini ya miaka 28 bila kujali jinsia yake.
  • Muongozo uandikwe ama kwa Kiswahili auKiingereza
  • Muongozo usizidi  kurasa kumi na usipungue kurasa saba. (filamu fupi)
  • Muongozo uchapishwe katika mfumo huu: Ukubwa wa Maneno (font size 12) Mfumo wa maneno (Courier or a slight variation (Courier Prime or Courier New).
  • Mada kuu ya mwaka huu katika kipengere hiki ni “Mapambano ya matumizi ya dawa ya kulevya kwa vijana nchini Tanzania). Miongozo yote ya filamu inabidi itumie mada kuu hii ya mwaka.

Zoezi la Mchujo:

Baada ya tarehe ya mwisho ya kutuma kazi, kazi zote zita pitiwa na jopo la majaji  na kupatikana watu ishirini, hawa ishirini watatakiwa kuja kuelezea mbele ya majaji kuhusu muongozo wao ambapo watatno watachaguliwa kuingia katika hatua inayofuata. Watano hawa watashiriki siku sita za kambi na kupewa mafunzo zaidi ya kuboresha kazi zao na siku ya mwisho  ya kambi watatakiwa kuelezea tena kazi zao mbele ya majaji na watatu watachaguliwa kuingia fainali. Ambapo siku ya fainali mshindi atatangazwa.

Kutuma kazi yako:

  • Kila mshiriki atume kazi yake ikiwa katika mfumo wa PDF na endapo itakuwa imechapishwa katika mfumo wa Celtx script writing studio pia inaruhusuiwa kutuma ikiwa katika mfumo wake wa awali/halisi (original).

Angalizo: Washiriki waliopita katika mashindano ya FASDO hawaruhusiwi kushiriki.

Tuma Kazi yako Hapa!

Go to top