Mpiga picha kijana

Mpiga picha kijana

Kipengele hiki kinalenga kutafuta vijana wenye kipaji cha upigaji picha na wenye mapenzi ya kazi ya upigaji picha. Washiriki katika kipengere hiki wanatakiwa:

  • Kuwa raia wa Tanzania mwenye umri usiozidi miaka 28 wakati wa kujiandikisha kushiriki shindano.
  • Mwenye mapenzi ya dhati ya kuwa mpiga picha.
  • Awe ana kamera yake mwenyewe
  • Anatakiwa kutuma picha zake tatu au tano (zinaweza kuwa ni picha za habari/kiuandishi, au zinaonyesha fahari ya mwafrika katika tamaduni au sanaa za kiafrika au mchanganyiko wa vyote).
  • Kazi  zote lazima ziakisi kauli mbiu: KILA SIKU TANZANIA
  • Picha iwe na Ukubwa usiopungua 1500px kwenye urefu na usiozidi 3000px kwenye urefu
  • Lila picha ni lazima iwe na kichwa cha habari na maelezo na pia iweze kujieleza.

KUMBUKA: Washindi wa mashindano yaliyopita ya FASDO hawaruhusiwi kushiriki.

Tuma kazi yako hapa!

Go to top