Bongo Style Ushindani

Kuhusu Mradi

Bongo Style Competition 2017 Mimi ni mwafrika inalenga kutambua, kutoa tuzo/zawadi na kusapoti wabunifu mitindo vijana, wapiga picha vijana na waandishi wa filamu vijana na kuhamasisha vijana kuongeza thamani katika sanaa na tamaduni za kiafrika. Bongo Style Competition 2017 ni kwa ajili ya vijana wenye umri wa miaka usiozidi miaka 28. Shindano lina vipengere vitatu: Mbunifu Mitindo bora kijana, Mpiga picha bora kijana na mwandishi wa filamu bora kijana. Wote wenye umri wa miaka 28 na kushuka chini.

Vigezo na Masharti

Shindano ni kwa vijana  wa kitanzania tu wenye umri usiozidi miaka 28. Vigezo na masharti yafuatayo yatazingatiwa wakati wa tathmini:

 • Ubunifu, kujieleza, upekee na usafi wa kazi/muonekano wa kazi.
 • Kazi zote ziongelee tamaduni za kiafrika, urithi/amali na hali halisi ya kiafrika. Iwe inayoakisi kauli mbinu: MIMI NI MWAFRIKA 
 • Iwe inayoweza kuchapishwa (isiwe inayokiuka maadili, isiwe na udhalilishaji wa aina yoyote) na isiwe imewahi kuchapishwa/kutolewa au kushindanishwa kwenye mashindano mengine kabla
 • Iwe kazi iliyofanyiwa utafiti wa kutosha.
 • Kazi iwe ni ya ubunifu wa mshiriki kwa asilimia 100%.

KUMBUKA: Vigezo na masharti mengine yapo kwenye maelezo ya kila kipengere cha ushindani. 

Muongozo

 • Jinsi/namna ya kushiriki:
  • soma vigezo na  masharti vizuri.
  • Tengeneza kazi yako kwa kuzingatia vigezo na masharti
  • Kazi zako zote (picha na video weka katika folder moja)
  • Hakikisha umeandika taarifa zako zote kiusahihi kabla ya kubonyeza kifute cha kutuma (submit)
  • Itume kazi yako (fomu ya kutuma kazi)
 • kila kazi lazima iwe na kichwa cha habari.
 • ushiriki wote lazima uzingatie uelewa wa taarifa za vigezo na masharti ya shindano.

Tarehe za Mwisho wa Kushiriki

 • Tarehe  30 mwezi wa tano: mwisho wa kutuma kazi.
 • Tarehe 15 mwezi wa sita: Kutangaza 25 bora.
 • Tarehe  28 – 30 mwezi wa sita - Mafunzo kwa washiriki 25 bora.
 • Tarehe 1- 6 mwezi wa saba – kambi
 • Tarehe 3  mwezi wa saba – kutangaza kumi  na tatu bora kwa ajili ya fainali.
 • Tarehe 3 hadi 6 mwezi wa saba: Upigaji kura kwenye mtandao.
 • Tarehe 7 mwezi wa saba: Kutangaza washindi

Zawadi

mshindi wa kila kipengere (Mbunifu mitindo, mpiga picha na mwandishi wa filamu) atajishindia Tsh milioni moja pesa taslimu kama mtaji. Mwandishi wa Filamu bora atapata nafasi ya kutengeneza filamu yake itakayoenda kuonyeshwa katika maonyesho ya filamu maarufu kama Afrika Film Festival nchini Belgium mwaka 2018.Washiriki wote waliongia fainali  watapatiwa misaada mbalimbali katika kuendeleza vipaji vyao. Msaada huu utakuwa katika kuwatangaza, kuwakuza, na kusaidia umiliki wa kazi zao kisheria.

Go to top