Blogs

SHINDANO LA BONGO STYLE COMPETITION LAANZA!

Mwanzo wa wiki hii, shindano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa la BONGO STYLE COMPETITION limeanza rasmi. Shindano hilo linalotegemewa kuibua vipaji mbalimbali vya vijana wa kitanzania wenye umri kati ya miaka 18-25, lina vipengele viwili vya mpiga picha kijana na mbunifu wa mitindo ya mavazi kijana. Washindi wawili, mmoja kutoka kila kipengele, watajishindia Milioni moja kila mmoja na safari ya kwenda Ubelgiji kuonesha kazi zao ifikapo mwakani mwezi wa tatu. Pia washiriki bora 20 walioingia fainali watapata mafunzo na kusaidiwa kukuza vipaji vyao na kazi zao kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Pages

Subscribe to RSS - blogs
Go to top