January 2016

JIJUE

✨FASDO TANZANIA✨ SIKU TATU ZA KUJIJUA 2016 #JIJUE SIKU 1 A. MIMI ni NANI? Kuna tofauti kati ya jinsi watu wanavyokufahamu na jinsi halisi ulivyo. Kuna namna watu wanavyokuita na kuna namna jinsi ulivyo. Kuna namna watu wanavyokufikiria na jinsi vile ulivyo. Ili uyafikie mafanikio, ni lazima ufahamu WEWE ni nani ili uendelee kuwa hivyo au ubadilike. Mtu halisi ni yule ambaye unakuwa pale unapokuwa peke yako. Matendo halisi ni yale unayotenda pale ambapo hakuna anayekuona wala hakuna atakayegundua kuhusu ulilofanya. Huyu ndio wewe halisi. #jijue
Go to top